2 Timothy 3:13
Lakini watu waovu na wadanganyaji watazidi kuwa waovu, wakidanganya na kudanganyika.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
But evil men and seducers shall wax worse and worse, deceiving, and being deceived.
In Context
12Naam, yeyote anayetaka kuishi maisha ya utauwa ndani ya Kristo Yesu atateswa.
Cross References
Isaiah 44:20Hujilisha kwa majivu, moyo uliodanganyika humpotosha; 2 hawezi kujiokoa mwenyewe, au kusema, 2 “Je, kitu hiki kilichoko katika mkono wangu wa kuume si ni uongo?” 1
Ezekiel 14:9“ ‘Naye nabii kama atakuwa ameshawishika kutoa unabii, Mimi Bwana nitakuwa nimemshawishi nabii huyo, nami nitaunyoosha mkono wangu dhidi yake na kumwangamiza kutoka miongoni mwa watu wangu Israeli.
1 Timothy 4:1Roho asema waziwazi kwamba katika siku za mwisho baadhi ya watu wataiacha imani na kufuata roho zidanganyazo na mafundisho ya mashetani.
2 Timothy 3:8Kama vile Yane na Yambre walivyopingana na Mose, vivyo hivyo watu hawa hupingana na ile kweli. Hawa ni watu wenye akili zilizopotoka, ambao wamekataliwa kwa mambo ya imani.
2 Peter 2:20Kama wameukimbia upotovu wa dunia kwa kumjua Bwana wetu na Mwokozi Yesu Kristo, kisha wakanaswa tena humo na kushindwa, hali yao ya mwisho ni mbaya zaidi kuliko ile ya kwanza.
Revelation 12:9Lile joka kuu likatupwa chini, yule nyoka wa zamani aitwaye ibilisi au Shetani, aupotoshaye ulimwengu wote. Akatupwa chini duniani, yeye pamoja na malaika zake. 1 Ushindi Mbinguni Watangazwa