Acts 15:3
Hivyo wakasafirishwa na kanisa, wakiwa njiani wakapitia nchi ya Foinike na Samaria, wakawaeleza jinsi watu wa Mataifa walivyookoka. Habari hizi zikaleta furaha kubwa kwa ndugu wote.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Isaiah 66:12Kwa kuwa hili ndilo asemalo Bwana: 1 “Nitamwongezea amani kama mto, 2 nao utajiri wa mataifa kama kijito kifurikacho; 1 utanyonya na kuchukuliwa mikononi mwake 2 na kubembelezwa magotini pake. 1
Luke 15:23Leteni ndama aliyenona, mkamchinje ili tuwe na karamu, tule na kufurahi.
Acts 8:14Basi mitume waliokuwa Yerusalemu waliposikia kuwa Samaria wamelipokea neno la Mungu, wakawatuma Petro na Yohana waende huko.
Acts 13:48Watu wa Mataifa waliposikia haya wakafurahi na kulitukuza neno la Bwana; nao wote waliokuwa wamekusudiwa uzima wa milele wakaamini.
Acts 14:27Walipowasili Antiokia wakaliita kanisa pamoja na kutoa taarifa ya yale yote Mungu aliyokuwa ametenda kupitia kwao na jinsi alivyokuwa amefungua mlango wa imani kwa ajili ya watu wa Mataifa.
Acts 21:5Lakini muda wetu ulipokwisha, tukaondoka tukaendelea na safari yetu. Wale wanafunzi pamoja na wake zao na watoto wakatusindikiza hadi nje ya mji. Wote tukapiga magoti pale pwani tukaomba.