Acts 16:34
Akawapandisha nyumbani mwake akawaandalia chakula, yeye pamoja na nyumba yake yote wakafurahi sana kwa kuwa sasa walikuwa wamemwamini Mungu.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Isaiah 55:12Mtatoka nje kwa furaha 2 na kuongozwa kwa amani; 1 milima na vilima 2 vitapaza sauti kwa nyimbo mbele yenu, 1 nayo miti yote ya shambani 2 itapiga makofi. 1
Isaiah 58:7Je, sio kushirikiana chakula chako na wenye njaa 2 na kuwapatia maskini wasiokuwa na makao hifadhi, 1 unapomwona aliye uchi, umvike, 2 wala si kumkimbia mtu wa nyama na damu yako mwenyewe? 1
Luke 5:29Kisha Lawi akamfanyia Yesu karamu kubwa nyumbani kwake, nao umati mkubwa wa watoza ushuru na watu wengine walikuwa wakila pamoja nao.
Luke 15:32Lakini ilitubidi tufurahi na kushangilia kwa sababu huyu ndugu yako alikuwa amekufa na sasa yu hai; alikuwa amepotea naye amepatikana.’ ”
Acts 2:46Siku zote kwa moyo mmoja walikutana ndani ya ukumbi wa Hekalu, wakimega mkate nyumba kwa nyumba, wakila chakula chao kwa furaha na moyo mweupe,
Acts 11:14Yeye atakupa ujumbe ambao kwa huo wewe na wa nyumbani mwako wote mtaokoka.’