Acts 16:5
Hivyo makanisa yakawa imara katika imani na kuongezeka kiidadi kila siku.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
And so were the churches established in the faith, and increased in number daily.
In Context
Cross References
2 Chronicles 20:20Asubuhi na mapema wakaondoka kuelekea Jangwa la Tekoa. Walipoanza safari, Yehoshafati akasimama akasema, “Nisikilizeni, enyi Yuda, na watu wa Yerusalemu! Mwaminini Bwana Mungu wenu, hivyo mtathibitika, wasadikini manabii wake nanyi mtafanikiwa.
Acts 2:47wakimsifu Mungu na kuwapendeza watu wote. Kila siku Bwana akaliongeza kanisa wale waliokuwa wakiokolewa.
Acts 5:14Hata hivyo, waliomwamini Bwana wakazidi kuongezeka, wanaume na wanawake.
Acts 9:31Ndipo kanisa katika Uyahudi wote, Galilaya na Samaria likafurahia wakati wa amani. Likatiwa nguvu, na kwa faraja ya Roho Mtakatifu, idadi yake ikazidi kuongezeka, na likaendelea kudumu katika kumcha Bwana. 1 Matendo Ya Petro (9:32–12:25) 1 Kuponywa Kwa Ainea
Acts 12:24Lakini neno la Mungu likaendelea mbele na kuenea, nao wengi wakaambatana nalo.
Acts 15:41Akapitia Shamu na Kilikia, akiimarisha makanisa ya huko.