Acts 17:24
“Mungu aliyeumba dunia na vyote vilivyomo ndani yake, yeye ndiye Bwana wa mbingu na nchi, hakai katika mahekalu yaliyojengwa kwa mikono ya wanadamu.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Genesis 14:19Naye akambariki Abramu, akisema, 1 “Abarikiwe Abramu na Mungu Aliye Juu Sana, 2 Muumba wa mbingu na nchi. 1
Deuteronomy 10:14Mbingu, hata mbingu za juu sana, dunia na kila kitu kilichomo ndani yake, ni mali ya Bwana Mungu wako.
2 Kings 19:15Naye Hezekia akamwomba Bwana akisema: “Ee Bwana, Mungu wa Israeli, uketiye juu ya kiti cha enzi kati ya makerubi, wewe peke yako ndiwe Mungu juu ya falme zote za dunia. Wewe umeumba mbingu na nchi.
2 Chronicles 6:18“Lakini kweli, je, Mungu atafanya makao duniani na wanadamu? Mbingu, hata mbingu zilizo juu sana, haziwezi kukutosha wewe. Sembuse Hekalu hili nililojenga!
Psalms 115:16Mbingu zilizo juu sana ni mali ya Bwana, 2 lakini dunia amempa mwanadamu. 1
Psalms 148:13Wote na walisifu jina la Bwana, 2 kwa maana jina lake pekee limetukuka, 2 utukufu wake uko juu ya nchi na mbingu. 1