Acts 18:24
Basi akaja Efeso Myahudi mmoja, jina lake Apolo, mwenyeji wa Iskanderia. Yeye alikuwa na elimu kubwa, pia alikuwa hodari katika Maandiko.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Ezra 7:6Huyu Ezra alipanda kutoka Babeli. Alikuwa mwalimu mwenye ujuzi mzuri katika sheria ya Mose, ambayo Bwana, Mungu wa Israeli, alikuwa ametoa. Mfalme alikuwa amempa Ezra kila kitu alichoomba, kwa maana Bwana Mungu wake alikuwa pamoja naye.
Isaiah 3:3jemadari wa kikosi cha watu hamsini 2 na mtu mwenye cheo, mshauri, 2 fundi stadi na mlozi mjanja. 1
Luke 24:19Akawauliza, “Mambo gani?” Wakamjibu, “Mambo ya Yesu wa Nazareti. Yeye alikuwa nabii, mwenye uwezo mkuu katika maneno yake na matendo yake, mbele za Mungu na mbele ya wanadamu wote.
Acts 7:22Mose akafundishwa hekima yote ya Wamisri, akawa mtu hodari kwa maneno na matendo.
Acts 27:6Huko yule kiongozi wa askari akapata meli ya Iskanderia ikielekea Italia, akatupandisha humo.
1 Corinthians 2:1Ndugu zangu nilipokuja kwenu, sikuja na maneno ya ushawishi wala hekima ya hali ya juu nilipowahubiria siri ya Mungu.