Acts 20:17
Paulo akiwa Mileto, alituma mjumbe kwenda Efeso kuwaita wazee wa kanisa waje wakutane naye.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
And from Miletus he sent to Ephesus, and called the elders of the church.
In Context
Cross References
Acts 11:30Wakafanya hivyo, misaada yao ikapelekwa kwa wazee kwa mikono ya Barnaba na Sauli.
Acts 15:4Walipofika Yerusalemu, walipokelewa na kanisa na mitume pamoja na wazee, ndipo Paulo na Barnaba wakawaarifu kila kitu Mungu alichokuwa amefanya kupitia kwao.
Acts 15:23Wakatumwa na barua ifuatayo: Sisi mitume na wazee, ndugu zenu, Kwa ndugu Mataifa mlioamini mlioko Antiokia, Shamu na Kilikia: Salamu.
Acts 20:28Jilindeni nafsi zenu na mlilinde lile kundi lote ambalo Roho Mtakatifu amewaweka ninyi kuwa waangalizi wake. Lichungeni kanisa lake Mungu alilolinunua kwa damu yake mwenyewe.
Titus 1:5Sababu ya mimi kukuacha huko Krete ni ili uweke utaratibu mambo yale yaliyosalia na kuwaweka wazee wa kanisa katika kila mji, kama nilivyokuagiza.
1 Peter 5:1Kwa wazee waliomo miongoni mwenu, nawasihi mimi nikiwa mzee mwenzenu, shahidi wa mateso ya Kristo, na mshiriki katika utukufu utakaofunuliwa: