Acts 7:34
Hakika nimeona mateso ya watu wangu huko Misri. Nimesikia kilio chao cha uchungu, nami nimeshuka ili niwaokoe. Basi sasa njoo, nami nitakutuma Misri.’
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
33“Ndipo Bwana akamwambia, ‘Vua viatu vyako kwa maana mahali unaposimama ni patakatifu.
Cross References
Genesis 11:7Njooni, tushuke tuvuruge lugha yao ili wasielewane wao kwa wao.”
Exodus 2:23Baada ya muda mrefu, mfalme wa Misri akafa. Waisraeli wakalia kwa huzuni katika utumwa wao, walilia na kilio chao cha kutaka msaada kwa ajili ya utumwa kikamfikia Mungu.
Exodus 3:14Mungu akamwambia Mose, “ Mimi niko ambaye niko. Hivyo ndivyo utakavyowaambia Waisraeli: ‘ Mimi niko amenituma kwenu.’ ”
Exodus 6:5Zaidi ya hayo, nimesikia kilio cha huzuni cha Waisraeli ambao Wamisri wamewatia utumwani, nami nimelikumbuka Agano langu.
Judges 2:18Kila mara Bwana alipowainulia mwamuzi, Bwana alikuwa pamoja na huyo mwamuzi, naye aliwaokoa kutoka mikononi mwa adui zao kwa kipindi chote alichoishi yule mwamuzi. Kwa kuwa Bwana aliwahurumia kwa sababu ya kilio chao cha huzuni kwa ajili ya wale waliokuwa wakiwatesa na kuwataabisha.
Nehemiah 9:9“Uliona mateso ya baba zetu huko Misri, ukasikia kilio chao huko Bahari ya Shamu.