Acts 9:4
Akaanguka chini, akasikia sauti ikimwambia, “Sauli, Sauli, mbona unanitesa?”
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
And he fell to the earth, and heard a voice saying unto him, Saul, Saul, why persecutest thou me?
In Context
5Sauli akajibu, “U nani wewe, Bwana?” Ile sauti ikajibu, “Mimi ni Yesu unayemtesa.
Cross References
Genesis 3:9Lakini Bwana Mungu akamwita Adamu, “Uko wapi?”
Genesis 22:11Lakini malaika wa Bwana akamwita kutoka mbinguni, akamwambia, “Abrahamu! Abrahamu!” Akajibu, “Mimi hapa.”
Numbers 16:45“Jitenge mbali na kusanyiko hili ili niweze kuwaangamiza mara moja.” Wakaanguka chini kifudifudi.
Zechariah 2:8Kwa kuwa hivi ndivyo asemavyo Bwana Mwenye Nguvu Zote: “Baada ya yeye kuniheshimu na kunituma mimi dhidi ya mataifa yaliyokuteka nyara, kwa kuwa yeyote awagusaye ninyi, anaigusa mboni ya jicho lake,
Matthew 25:45“Naye atawajibu, ‘Amin nawaambia, kwa jinsi ambavyo hamkumtendea mmojawapo wa hawa ndugu zangu walio wadogo, hamkunitendea mimi.’
John 18:6Yesu alipowaambia, “Mimi ndiye,” walirudi nyuma na kuanguka chini!