Amosi 5:15
Yachukieni maovu, yapendeni mema; 2 dumisheni haki mahakamani. 1 Yamkini Bwana Mungu Mwenye Nguvu Zote 2 atawahurumia mabaki ya Yosefu.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Exodus 32:30Siku iliyofuata Mose akawaambia watu, “Mmefanya dhambi kubwa. Lakini sasa nitapanda juu kwa Bwana, labda nitaweza kufanya upatanisho kwa ajili ya dhambi yenu.”
1 Kings 20:31Maafisa wake wakamwambia, “Tazama, tumesikia kwamba wafalme wa nyumba ya Israeli wana huruma. Twendeni kwa mfalme wa Israeli tukiwa tumevaa nguo za gunia viunoni mwetu na kamba kuzunguka vichwa vyetu. Huenda akakuacha hai.”
2 Kings 14:26Bwana alikuwa ameona jinsi kila mmoja katika Israeli, awe mtumwa au aliye huru, alivyoteseka kwa uchungu; hapakuwepo na yeyote wa kuwasaidia.
2 Kings 19:4Yamkini Bwana, Mungu wako atayasikia maneno ya jemadari wa jeshi, ambaye bwana wake, mfalme wa Ashuru, amemtuma kumdhihaki Mungu aliye hai, tena kwamba atamkemea kwa maneno ambayo Bwana, Mungu wako ameyasikia. Kwa hiyo omba kwa ajili ya mabaki ambao bado wako.”
Psalms 34:14Aache uovu, atende mema, 2 aitafute amani na kuifuatilia. 1
Psalms 37:27Acha ubaya na utende wema, 2 nawe utaishi katika nchi milele. 1