Amosi 6:14
Maana Bwana Mungu Mwenye Nguvu Zote asema, 2 “Nitainua taifa dhidi yenu, ee nyumba ya Israeli, 1 nalo litawatesa kuanzia Lebo-Hamathi 2 hadi Bonde la Araba.”
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
1 Kings 8:65Hivyo Solomoni akaiadhimisha sikukuu kwa wakati ule, na Israeli wote pamoja naye. Walikuwa kusanyiko kubwa sana, watu kutoka Lebo-Hamathi hadi Kijito cha Misri. Wakaiadhimisha mbele za Bwana Mungu wetu kwa siku saba na siku saba zaidi, yaani, jumla siku kumi na nne.
2 Kings 15:29Wakati wa utawala wa Peka mfalme wa Israeli, Tiglath-Pileseri mfalme wa Ashuru alikuja na kuteka Iyoni, Abel-Beth-Maaka, Yanoa, Kedeshi na Hazori. Akateka miji ya Gileadi na Galilaya, pamoja na nchi yote ya Naftali, na kuwahamishia watu wote Ashuru.
Isaiah 7:20Katika siku ile Bwana atatumia wembe ulioajiriwa kutoka ngʼambo ya Mto, + 7:20 Yaani Frati. yaani mfalme wa Ashuru, kunyoa nywele za kichwa chako na malaika ya miguu yako, na kuziondoa ndevu zako pia.
Isaiah 10:5“Ole kwa Ashuru, fimbo ya hasira yangu, 2 ambaye mkononi mwake ana rungu ya ghadhabu yangu! 1
Ezekiel 47:15“Huu ndio utakuwa mpaka wa hiyo nchi: 1 “Upande wa kaskazini utaanzia Bahari Kuu kwa njia ya Hethloni kupitia Lebo-Hamathi hadi maingilio ya Sedadi.