Daniel 10:19
Akasema, “Ee mtu upendwaye sana, usiogope. Amani iwe kwako! Uwe na nguvu sasa; jipe nguvu.” Alipozungumza nami, nilipata nguvu, nikasema, “Nena, bwana wangu, kwa kuwa umenipa nguvu.”
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
18Tena yule aliyeonekana kama mwanadamu akanigusa na kunitia nguvu.
Cross References
Joshua 1:6“Uwe hodari na shujaa, kwa sababu wewe ndiwe utakayewaongoza watu hawa kuirithi nchi niliyowaapia baba zao kuwapa.
Judges 6:23Lakini Bwana akamwambia, “Amani iwe kwako! Usiogope. Hutakufa.”
Psalms 138:3Nilipoita, ulinijibu; 2 ulinifanya jasiri na mwenye moyo hodari. 1
Isaiah 41:10Hivyo usiogope, kwa maana niko pamoja nawe; 2 usifadhaike, kwa maana mimi ni Mungu wako. 1 Nitakutia nguvu na kukusaidia; 2 nitakutegemeza kwa mkono wa kuume wa haki yangu. 1
Isaiah 43:1Lakini sasa hili ndilo asemalo Bwana, 2 yeye aliyekuumba, ee Yakobo, 2 yeye aliyekuhuluku, ee Israeli: 1 “Usiogope kwa maana nimekukomboa, 2 nimekuita wewe kwa jina lako, wewe u wangu. 1
Daniel 10:11Akasema, “Danieli, wewe mtu upendwaye sana, fikiri kwa makini maneno ninayokwenda kunena nawe sasa; simama wima, kwa maana sasa nimetumwa kwako.” Naye aliponiambia haya, nikasimama nikitetemeka.