Isaiah 41:10
Hivyo usiogope, kwa maana niko pamoja nawe; 2 usifadhaike, kwa maana mimi ni Mungu wako. 1 Nitakutia nguvu na kukusaidia; 2 nitakutegemeza kwa mkono wa kuume wa haki yangu. 1
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Genesis 15:1Baada ya jambo hili, neno la Bwana likamjia Abramu katika maono: 1 “Usiogope, Abramu. 2 Mimi ni ngao yako, 2 na thawabu yako kubwa sana.”
Exodus 14:13Mose akawajibu Waisraeli, “Msiogope. Simameni imara, nanyi mtauona wokovu Bwana atakaowapatia leo. Hao Wamisri mnaowaona leo kamwe hamtawaona tena.
Deuteronomy 31:6Kuweni imara na moyo wa ushujaa. Msiogope wala msifadhaike kwa sababu yao, kwa kuwa Bwana Mungu wenu anakwenda pamoja nanyi; kamwe hatawaacha wala hatawatupa ninyi.”
Joshua 1:9Je, si mimi niliyekuamuru? Uwe hodari na shujaa. Usihofu wala usivunjike moyo, kwa kuwa Bwana Mungu wako atakuwa pamoja nawe kokote uendako.”
2 Samuel 22:19Walinikabili siku ya msiba wangu, 2 lakini Bwana alikuwa msaada wangu. 1
2 Chronicles 20:17Hamtahitaji kupigana vita hivi. Kaeni kwenye nafasi zenu, simameni imara na mkaone wokovu Bwana atakaowapatia, enyi Yuda na Yerusalemu. Msiogope, wala msifadhaike. Kesho tokeni mwende mkawakabili, naye Bwana atakuwa pamoja nanyi.’ ”