Daniel 11:16
Huyo mvamia nchi atafanya apendavyo; hakuna yeyote atakayeweza kumpinga. Atajiimarisha katika Nchi ya Kupendeza, na atakuwa na uwezo wa kuiangamiza.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Joshua 1:5Hakuna mtu yeyote atakayeweza kushindana na wewe siku zote za maisha yako. Kama vile nilivyokuwa pamoja na Mose, ndivyo nitakavyokuwa pamoja na wewe, sitakuacha wala sitakupungukia.
Jeremiah 3:19“Mimi mwenyewe nilisema, 1 “ ‘Tazama jinsi nitakavyowatunza kwa furaha kama wana 2 na kuwapa nchi nzuri, 2 urithi ulio mzuri kuliko wa taifa jingine lolote.’ 1 Nilidhani mngeniita ‘Baba,’ 2 na msingegeuka, mkaacha kunifuata. 1
Daniel 8:7Nikamwona akimshambulia yule kondoo dume kwa hasira nyingi, akimpiga yule kondoo dume na kuvunja pembe zake mbili. Yule kondoo dume hakuwa na nguvu za kumzuia yule beberu, hivyo akamwangusha yule kondoo dume chini na kumkanyaga, wala hakuna aliyeweza kumwokoa yule kondoo dume kutoka nguvu za huyo beberu.
Daniel 11:3Ndipo mfalme mwenye nguvu atatokea, ambaye atatawala kwa nguvu nyingi na kufanya anavyopenda.
Daniel 11:41Pia ataivamia Nchi ya Kupendeza. Nchi nyingi zitapinduliwa, bali Edomu, Moabu na viongozi wa Amoni wataokolewa kutoka mkono wake.