Daniel 4:1
Mfalme Nebukadneza, Kwa kabila za watu, mataifa na watu wa kila lugha, wanaoishi katika ulimwengu wote: Mafanikio yawe kwenu sana!
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
1 Chronicles 12:18Kisha Roho akaja juu ya Amasai, mkuu wa wale Thelathini, naye akasema: 1 “Sisi tu watu wako, ee Daudi! 2 Nasi tuko pamoja na wewe, ee mwana wa Yese! 1 Ushindi, naam, ushindi uwe kwako, 2 pia ushindi kwa wale walio upande wako, 3 kwa kuwa Mungu wako atakusaidia.” Kwa hiyo Daudi akawapokea na kuwafanya viongozi wa vikosi vyake vya uvamizi.
Ezra 5:7Taarifa waliyompelekea ilisomeka kama ifuatavyo: Kwa Mfalme Dario: Salamu kwa moyo mkunjufu.
Esther 8:9Mara moja waandishi wa mfalme wakaitwa kwenye siku ya ishirini na tatu, mwezi wa tatu, ndio mwezi wa Siwani. Wakaandika yote Mordekai aliyoamuru kwa Wayahudi, kwa majemadari, watawala na wakuu wa majimbo 127 kuanzia Bara Hindi mpaka Kushi. + 8:9 Kushi hapa ina maana ya Ethiopia. Maagizo haya yaliandikwa kwa maandishi ya kila jimbo na kwa lugha ya kila mtu pia kwa Wayahudi kwa maandishi yao wenyewe na lugha yao.
Daniel 3:29Kwa hiyo ninaamuru kwamba watu wa taifa lolote au lugha yoyote watakaosema kitu chochote dhidi ya Mungu wa Shadraki, Meshaki na Abednego wakatwe vipande vipande na nyumba zao zifanywe kuwa malundo ya kokoto, kwa maana hakuna mungu mwingine awezaye kuokoa namna hii.”
Daniel 6:27Huponya na kuokoa; 2 hufanya ishara na maajabu 2 mbinguni na duniani. 1 Amemwokoa Danieli 2 kutoka nguvu za simba.”
Zechariah 8:23Hili ndilo asemalo Bwana Mwenye Nguvu Zote: “Katika siku hizo watu kumi kutoka lugha zote na mataifa, watangʼangʼania upindo wa joho la Myahudi mmoja na kusema, ‘Twende pamoja nawe kwa sababu tumesikia kwamba Mungu yu pamoja nawe.’ ”