Daniel 4:8
Mwishoni, Danieli alikuja mbele yangu nikamweleza hiyo ndoto. (Danieli anaitwa Belteshaza, kwa jina la mungu wangu, nayo roho ya miungu mitakatifu inakaa ndani yake.)
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Isaiah 46:1Beli anasujudu hadi nchi, Nebo anainama; 2 sanamu zao zabebwa na wanyama wa mizigo. 1 Vinyago hivi mnavyobeba kila mahali ni mzigo wa kulemea, 2 mzigo kwa waliochoka. 1
Jeremiah 50:2“Tangazeni na mhubiri katikati ya mataifa, 2 twekeni bendera na mkahubiri; 2 msiache kitu chochote, bali semeni, 1 ‘Babeli utatekwa; 2 Beli ataaibishwa, 2 Merodaki atajazwa na hofu kuu. 1 Sanamu zake zitaaibishwa 2 na vinyago vyake vitajazwa hofu kuu.’ 1
Daniel 1:7Mkuu wa maafisa akawapa majina mapya: Danieli akamwita Belteshaza, Hanania akamwita Shadraki, Mishaeli akamwita Meshaki, na Azaria akamwita Abednego.
Daniel 4:9Nilisema, “Belteshaza, mkuu wa waganga, ninajua kuwa roho ya miungu mitakatifu iko ndani yako, wala hakuna siri iliyo ngumu kwako. Hii ndiyo ndoto yangu, nifasirie.
Daniel 5:11Yuko mtu katika ufalme wako ambaye ana roho ya miungu mitakatifu ndani yake. Wakati wa baba yako, mtu huyo alionekana kuwa na ufahamu, akili na hekima kama ile ya miungu. Mfalme Nebukadneza baba yako, yaani nasema mfalme baba yako, alimweka kuwa mkuu wa waganga, wasihiri, wanajimu na waaguzi.