Kumbukumbu 17:20
naye asijifikirie kuwa ni bora kuliko ndugu zake na kuipotosha sheria. Ndipo yeye na wazao wake watatawala katika ufalme wake kwa muda mrefu katika Israeli.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Deuteronomy 4:2Usiongeze wala usipunguze chochote ninachowaamuru ninyi, ila myashike maagizo ya Bwana Mungu wenu ambayo nawapa.
Deuteronomy 8:2Kumbuka jinsi Bwana Mungu wenu alivyowaongoza katika njia yote katika jangwa kwa miaka hii arobaini, kukunyenyekeza na kukujaribu ili ajue lililoko moyoni mwako, kwamba utayashika maagizo yake au la.
Deuteronomy 12:25Msinywe damu, ili mweze kufanikiwa ninyi pamoja na watoto wenu baada yenu, kwa sababu mtakuwa mkifanya lililo haki machoni pa Bwana.
Deuteronomy 12:32Angalieni kwamba mnafanya yote niliyowaamuru; msiongeze kitu wala msipunguze kitu.
1 Samuel 10:25Samweli akawaeleza watu madaraka ya ufalme. Akayaandika kwenye kitabu na kuweka mbele za Bwana. Kisha Samweli akawaruhusu watu, kila mmoja aende nyumbani kwake.
1 Samuel 15:23Kwa maana kuasi ni kama dhambi ya uaguzi, 2 nao ukaidi ni kama uovu wa kuabudu sanamu. 1 Kwa sababu umelikataa neno la Bwana, 2 naye amekukataa wewe 2 kuendelea kuwa mfalme.”