Kumbukumbu 28:62
Ninyi ambao mlikuwa wengi kama nyota za angani mtaachwa wachache tu, kwa sababu hamkumtii Bwana Mungu wenu.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Deuteronomy 1:10Bwana Mungu wenu ameongeza hesabu yenu, hivi kwamba leo ninyi ni wengi kama nyota za angani.
Deuteronomy 4:27Bwana atawatawanya miongoni mwa mataifa, na ni wachache wenu tu watakaosalia miongoni mwa mataifa hayo ambayo Bwana atawafukuzia.
2 Kings 13:7Hapakubaki kitu chochote katika jeshi la Yehoahazi isipokuwa wapanda farasi hamsini, magari kumi ya vita na askari wa miguu elfu kumi, kwa kuwa mfalme wa Aramu alikuwa amewaangamiza hao wengine na kuwafanya kama mavumbi wakati wa kupura nafaka.
Nehemiah 7:4Mji ulikuwa mkubwa, tena wenye nafasi nyingi, lakini walikuwepo watu wachache ndani yake, nazo nyumba zilikuwa bado ni magofu.
Isaiah 1:9Kama Bwana Mungu Mwenye Nguvu Zote + 1:9 Bwana Mwenye Nguvu Zote hapa ni Yehova Sabaoth, yaani Bwana wa Majeshi; pia Warumi 9:29 na Yakobo 5:4. 2 asingelituachia walionusurika, 1 tungelikuwa kama Sodoma, 2 tungelifanana na Gomora. 1
Isaiah 6:13Hata kama sehemu ya kumi ya watu watabaki katika nchi, 2 itaharibiwa tena. 1 Lakini kama vile mvinje na mwaloni 2 ibakizavyo visiki inapokatwa, 2 ndivyo mbegu takatifu 2 itakavyokuwa kisiki katika nchi.”