Mhubiri 12:13
Hii ndiyo jumla ya maneno; 2 yote yamekwisha sikiwa: 1 Mche Mungu, nawe uzishike amri zake, 2 maana kwa jumla ndiyo impasayo mtu. 1
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
14Kwa maana Mungu ataleta hukumuni kila kazi, 2 pamoja na kila neno la siri, 2 likiwa jema au baya.
Cross References
Genesis 22:12Akamwambia, “Usimdhuru kijana, wala usimtendee jambo lolote. Sasa ninajua kwamba unamcha Mungu, kwa sababu hukunizuilia mwanao, mwana wako wa pekee.”
Deuteronomy 4:10Kumbuka siku uliyosimama mbele za Bwana Mungu wako kule Horebu, wakati aliponiambia, “Wakutanishe watu mbele yangu wasikie maneno yangu ili kwamba waweze kujifunza kuniheshimu kwa muda wote watakaoishi katika nchi, nao waweze kuwafundisha watoto wao maneno hayo.”
Deuteronomy 10:12Na sasa, ee Israeli, Bwana Mungu wako anataka nini kwako ila kumcha Bwana Mungu wako, kwenda katika njia zake, kumpenda na kumtumikia Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote na kwa roho yako yote,
1 Kings 2:3shika lile Bwana Mungu wako analokuagiza: Enenda katika njia zake, ushike maagizo na amri zake, sheria zake na kanuni zake, kama ilivyoandikwa katika Sheria ya Mose, ili upate kustawi katika yote ufanyayo na popote uendako,
Psalms 111:10Kumcha Bwana ndicho chanzo cha hekima, 2 wote wanaozifuata amri zake wana busara. 2 Sifa zake zadumu milele.
Psalms 145:19Huwatimizia wamchao matakwa yao, 2 husikia kilio chao na kuwaokoa. 1