Mhubiri 3:22
Kwa hiyo nikaona kwamba hakuna kitu kilicho bora zaidi kwa mwanadamu kuliko kuifurahia kazi yake, kwa sababu hilo ndilo fungu lake. Kwa maana ni nani awezaye kumrudisha ili aje kuona kile kitakachotendeka baada yake?
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
21Ni nani ajuaye kama roho ya mtu huenda juu na roho ya mnyama hushuka chini ardhini?”
Cross References
Deuteronomy 12:18Badala yake, mtakula vitu hivyo katika uwepo wa Bwana Mungu wenu mahali ambapo Bwana Mungu wenu atapachagua: wewe, wana wako na binti zako, watumishi wako wa kiume na wa kike, na Walawi kutoka miji yenu. Mnatakiwa mfurahi mbele za Bwana Mungu wenu kwa kula kitu mtakachoweka mikono yenu.
Deuteronomy 28:47Kwa sababu hukumtumikia Bwana Mungu wako kwa furaha na kwa moyo wakati wa kufanikiwa kwako,
Ecclesiastes 2:10Sikujinyima kitu chochote ambacho macho yangu yalikitamani, 2 hakuna anasa ambayo niliunyima moyo wangu. 1 Moyo wangu ulifurahia kazi zangu zote, 2 hii ilikuwa thawabu ya kazi zangu zote. 1
Ecclesiastes 3:11Amefanya kila kitu kiwe kizuri kwa wakati wake. Pia ameiweka hiyo milele katika mioyo ya wanadamu, wala hawawezi kutambua kwa kina yale ambayo Mungu amefanya tangu mwanzo hadi mwisho.
Ecclesiastes 5:18Ndipo nikatambua kwamba ni vyema na sahihi kwa mtu kula na kunywa na kutosheka katika kazi yake ngumu chini ya jua katika siku chache za maisha yake Mungu alizompa, kwa maana hili ndilo fungu lake.
Ecclesiastes 8:7Kwa vile hakuna mtu ajuaye siku zijazo, 2 ni nani awezaye kumwambia linalokuja? 1