Mhubiri 3:7
wakati wa kurarua na wakati wa kushona, 2 wakati wa kunyamaza na wakati wa kuzungumza, 2
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
A time to rend, and a time to sew; a time to keep silence, and a time to speak;
In Context
6wakati wa kutafuta na wakati wa kupoteza, 2 wakati wa kuweka na wakati wa kutupa, 2
8wakati wa kupenda na wakati wa kuchukia, 2 wakati wa vita na wakati wa amani.
Cross References
Genesis 37:29Reubeni aliporudi kutazama kwenye lile shimo na kuona kwamba Yosefu hayupo, alirarua nguo zake.
Genesis 44:18Ndipo Yuda akamwendea na kumwambia: “Tafadhali bwana wangu, mruhusu mtumishi wako aseme neno kwa bwana wangu. Usimkasirikie mtumishi wako, ingawa wewe ni sawa na Farao mwenyewe.
1 Samuel 10:16Sauli akajibu, “Alituhakikishia kwamba punda wamepatikana.” Lakini hakumwambia babaye mdogo kila kitu Samweli alichomwambia kuhusu ufalme.
1 Samuel 25:24Akamwangukia miguuni pake na kusema: “Bwana wangu, kosa hili na liwe juu yangu mwenyewe. Tafadhali mruhusu mtumishi wako aseme nawe. Sikia kile mtumishi wako atakachosema.
2 Samuel 3:31Kisha Daudi akamwambia Yoabu na watu wote aliokuwa pamoja nao, “Rarueni nguo zenu na mvae nguo za gunia na mtembee mkiomboleza mbele ya Abneri.” Mfalme Daudi mwenyewe akatembea nyuma ya jeneza.
2 Kings 5:7Mara mfalme wa Israeli alipomaliza kuisoma ile barua, akararua mavazi yake na kusema, “Je, mimi ni Mungu? Je, mimi naweza kuua na kufufua tena? Kwa nini huyu mtu anamtuma mtu ili mimi nipate kumponya ukoma wake? Tazama jinsi anavyotafuta kuanzisha ugomvi nami!”