Esta 5:14
Zereshi mkewe na rafiki zake wote wakamwambia, “Tengeneza mahali pa kuangika watu kimo chake dhiraa hamsini, + 5:14 Dhiraa 50 ni sawa na mita 22.5. kisha kesho asubuhi mwombe mfalme Mordekai aangikwe juu yake. Ndipo uende na mfalme kwenye karamu kwa furaha.” Shauri hili lilimpendeza Hamani, naye akajenga mahali pa kuangika watu.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
2 Samuel 13:3Basi Amnoni alikuwa na rafiki jina lake Yonadabu mwana wa Shimea, + 13:3 Shimea pia hutamkwa Shama. nduguye Daudi. Yonadabu alikuwa mtu wa hila nyingi sana.
1 Kings 21:7Yezebeli mke wake akasema, “Hivi ndivyo unavyofanya, nawe ni mfalme katika Israeli yote? Inuka na ule! Changamka. Nitakupatia shamba la mizabibu la Nabothi, Myezreeli.”
2 Chronicles 22:3Ahazia naye akaenenda katika njia za nyumba ya Ahabu, kwa sababu mama yake alimshawishi katika kutenda maovu.
Esther 6:4Mfalme akasema, “Ni nani yuko uani?” Wakati huo huo Hamani alikuwa ameingia ua wa nje wa jumba la mfalme kusema na mfalme kuhusu kumwangika Mordekai katika mahali pa kuangikia watu alipokuwa amepajenga kwa ajili yake.
Psalms 7:13Ameandaa silaha zake kali, 2 ameweka tayari mishale yake ya moto. 1
Psalms 37:14Waovu huchomoa upanga 2 na kupinda upinde, 1 ili wawaangushe maskini na wahitaji, 2 kuwachinja wale ambao njia zao ni nyofu. 1