Exodus 2:24
Mungu akasikia kilio chao cha huzuni, akakumbuka Agano alilofanya na Abrahamu pamoja na Isaki na Yakobo.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
25Kwa hiyo Mungu akawaangalia Waisraeli na kuwahurumia.
Cross References
Genesis 15:14Lakini nitaliadhibu taifa lile watakalolitumikia kama watumwa, na baadaye watatoka huko na mali nyingi.
Genesis 17:7Nitalithibitisha Agano langu kama Agano la milele kati yangu na wewe na wazao wako baada yako na vizazi vijavyo niwe Mungu wako na Mungu wa wazao wako.
Genesis 26:3Kaa katika nchi hii kwa kitambo, mimi nitakuwa pamoja na wewe na nitakubariki. Kwa maana nitakupa wewe na uzao wako nchi hizi zote na nitatimiza kiapo nilichomwapia Abrahamu baba yako.
Genesis 28:12Akaota ndoto ambayo aliona ngazi imesimamishwa juu ya ardhi, ncha yake ikiwa imefika mbinguni na malaika wa Mungu wakawa wakipanda na kushuka juu yake.
Genesis 32:28Ndipo yule mtu akasema, “Jina lako halitakuwa tena Yakobo, bali Israeli, + 32:28 Israeli maana yake Yeye ashindanaye na Mungu. kwa sababu umeshindana na Mungu na watu pia, nawe umeshinda.”
Genesis 35:12Nchi niliyowapa Abrahamu na Isaki nakupa wewe pia, nami nitawapa wazao wako baada yako.”