Kutoka 30:18
“Tengeneza sinia la shaba lenye kitako cha shaba kwa ajili ya kunawia. Liweke kati ya Hema la Kukutania na madhabahu, kisha uweke maji ndani yake.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
17Kisha Bwana akamwambia Mose,
19Aroni na wanawe watanawa mikono na miguu yao kwa maji yatokayo katika hilo sinia.
Cross References
Exodus 31:9madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa na vyombo vyake vyote, sinia na kinara chake,
Exodus 40:7weka sinia kati ya Hema la Kukutania na madhabahu, na uweke maji ndani yake.
Leviticus 8:11Akanyunyiza baadhi ya mafuta juu ya madhabahu mara saba, akaipaka madhabahu mafuta na vyombo vyake vyote pamoja na sinia na kinara chake, ili kuviweka wakfu.
1 Kings 7:38Kisha akatengeneza masinia kumi ya shaba, kila moja likiwa na ujazo wa bathi arobaini, + 7:38 Bathi 40 ni sawa na lita 800. yakiwa na kipenyo cha dhiraa nne + 7:38 Dhiraa nne ni sawa na mita 1.8. kila sinia moja kwa kila kimoja ya vile vitako kumi.
2 Chronicles 4:6Kisha akatengeneza masinia kumi kwa ajili ya kuoshea vifaa, naye akayaweka matano upande wa kusini na matano upande wa kaskazini. Ndani yake ndimo walioshea vifaa vya kutumika katika sadaka za kuteketezwa, lakini ile Bahari ilikuwa ni kwa ajili ya makuhani kunawia.
Zechariah 13:1“Katika siku hiyo, chemchemi itafunguliwa kwa nyumba ya Daudi na wakazi wa Yerusalemu, kuwatakasa dhambi na unajisi.