Kutoka 34:10
Kisha Bwana akasema: “Tazama ninafanya Agano mbele ya watu wako wote. Mbele ya watu wako wote nitafanya maajabu ambayo hayajafanyika katika taifa lolote katika ulimwengu wote. Watu wale mnaoishi miongoni mwao wataona jinsi ilivyo ya kushangaza ile kazi nitakayowafanyia mimi Bwana wenu.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Exodus 34:27Kisha Bwana akamwambia Mose, “Andika maneno haya, kwa maana kulingana na maneno haya, nimefanya Agano na wewe pamoja na Israeli.”
Deuteronomy 4:32Sasa uliza kuhusu siku za zamani, zamani kabla ya wakati wako, tangu siku ile Mungu alipomuumba mtu juu ya nchi, uliza kutoka mwisho mmoja wa mbingu mpaka mwisho mwingine wa mbingu. Je, kumepata kutokea jambo jingine lililo kubwa kama hili, au kuna jambo jingine kama hilo limepata kusikiwa?
Deuteronomy 10:21Yeye ni sifa yako; yeye ni Mungu wako, ambaye alikutendea yale maajabu makubwa na ya kutisha uliyoyaona kwa macho yako mwenyewe.
Deuteronomy 32:30Mtu mmoja angewezaje kufukuza elfu moja, 2 au wawili kufukuza elfu kumi, 1 kama si kwamba Mwamba wao amewauza, 2 kama si kwamba Bwana amewaacha? 1
Joshua 10:12Katika siku ile ambayo Bwana aliwapeana Waamori kwa Israeli, Yoshua akanena na Bwana akiwa mbele ya Waisraeli akasema: 1 “Wewe jua, simama juu ya Gibeoni, 2 wewe mwezi, tulia juu ya Bonde la Aiyaloni.” 1
Psalms 65:5Unatujibu kwa matendo ya kushangaza ya haki, 2 Ee Mungu Mwokozi wetu, 1 tumaini la miisho yote ya duniani 2 na la bahari zilizo mbali sana, 1