Ezekiel 39:21
“Nitauonyesha utukufu wangu miongoni mwa mataifa, nayo mataifa yote wataiona adhabu nitakayotoa na mkono wangu nitakaouweka juu yao.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
22Kuanzia siku ile na kuendelea nyumba ya Israeli itajua kuwa Mimi ndimi Bwana, Mungu wao.
Cross References
Exodus 8:19Waganga wale wakamwambia Farao, “Hiki ni kidole cha Mungu.” Lakini moyo wa Farao ukawa mgumu naye hakuwasikiliza, kama vile Bwana alivyosema. 1 Pigo La Nne: Mainzi
Exodus 14:4Nami nitaufanya moyo wa Farao mgumu, naye atawafuatilia. Lakini nitajipatia utukufu kwa ajili yangu mwenyewe kupitia Farao na jeshi lake lote, nao Wamisri watajua kuwa mimi ndimi Bwana.” Kwa hiyo Waisraeli wakafanya hivyo.
1 Samuel 5:11Basi wakawaita watawala wote wa Wafilisti pamoja na kusema, “Liondoeni Sanduku la Mungu wa Israeli na lirudishwe mahali pake, la sivyo litatuua sisi na watu wetu.” Kwa kuwa kifo kilikuwa kimeujaza mji hofu; kwani mkono wa Mungu ulikuwa mzito sana juu yake.
Psalms 32:4Usiku na mchana 2 mkono wako ulinilemea, 1 nguvu zangu zilinyonywa 2 kama vile katika joto la kiangazi. 1
Isaiah 26:11Ee Bwana, mkono wako umeinuliwa juu, 2 lakini hawauoni. 1 Wao na waone wivu wako kwa ajili ya watu wako tena waaibishwe, 2 moto uliowekwa akiba kwa ajili ya adui zako na uwateketeze. 1
Ezekiel 36:23Nitauonyesha utakatifu wa Jina langu kuu, ambalo limetiwa unajisi miongoni mwa mataifa, jina ambalo limetiwa unajisi miongoni mwao. Ndipo mataifa watakapojua kuwa Mimi ndimi Bwana, asema Bwana Mwenyezi, nitakapojionyesha mwenyewe kuwa mtakatifu kwa kuwapitia ninyi mbele ya macho yao.