Isaya 26:11
Ee Bwana, mkono wako umeinuliwa juu, 2 lakini hawauoni. 1 Wao na waone wivu wako kwa ajili ya watu wako tena waaibishwe, 2 moto uliowekwa akiba kwa ajili ya adui zako na uwateketeze. 1
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Exodus 9:14au wakati huu nitaleta mapigo yangu yenye nguvu dhidi yako, maafisa wako na watu wako, ili upate kujua kuwa hakuna mwingine kama Mimi katika dunia yote.
1 Samuel 6:9lakini liangalieni kwa makini. Iwapo litakwenda katika nchi yake lenyewe, kuelekea Beth-Shemeshi, basi tutajua kwamba Bwana ndiye alileta haya maafa makubwa juu yetu. Lakini kama halikwenda, basi tutajua kwamba haukuwa mkono wa Bwana uliotupiga na kwamba iliyotokea kwetu ni ajali.”
Psalms 10:12Inuka Bwana! Inua mkono wako, Ee Mungu. 2 Usiwasahau wanyonge. 1
Psalms 28:5Kwa kuwa hawaheshimu kazi za Bwana, 2 na yale ambayo mikono yake imetenda, 1 atawabomoa na kamwe 2 hatawajenga tena. 1
Isaiah 5:24Kwa hiyo, kama ndimi za moto zirambavyo nyasi, 2 na kama vile majani makavu yazamavyo katika miali ya moto, 1 ndivyo mizizi yao itakavyooza 2 na maua yao yatakavyopeperushwa kama mavumbi; 1 kwa kuwa wameikataa sheria ya Bwana Mwenye Nguvu Zote 2 na kulisukumia mbali neno la Aliye Mtakatifu wa Israeli. 1
Isaiah 11:13Wivu wa Efraimu utatoweka, 2 na adui wa Yuda watakatiliwa mbali; 1 Efraimu hatamwonea Yuda wivu, 2 wala Yuda hatakuwa na uadui na Efraimu. 1