Ezekieli 39:9
“ ‘Ndipo wale wanaoishi katika miji ya Israeli watakapotoka na kutumia hizo silaha kuwashia moto na kuziteketeza, yaani, kigao na ngao, pinde na mishale, rungu za vita na mikuki. Kwa miaka saba watavitumia kama kuni.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Psalms 46:9Anakomesha vita hata miisho ya dunia, 2 anakata upinde na kuvunjavunja mkuki, 2 anateketeza ngao kwa moto. 1
Isaiah 66:24“Nao watatoka nje na kuona maiti za wale walioniasi mimi. Funza wao hawatakufa, wala moto wao hautazimika, nao watakuwa kitu cha kuchukiza sana kwa wanadamu wote.”
Zechariah 9:10Nitaondoa magari ya vita kutoka Efraimu 2 na farasi wa vita kutoka Yerusalemu, 2 nao upinde wa vita utavunjwa. 1 Atatangaza amani kwa mataifa. 2 Utawala wake utaenea kutoka bahari hadi bahari, 2 na kutoka Mto Frati hadi mwisho wa dunia. 1