bible.software › Ezra › Ezra 5 › Ezra 5:13
Ezra 5:13
“Pamoja na hayo, katika mwaka wa kwanza wa kutawala Koreshi mfalme wa Babeli, Mfalme Koreshi alitoa amri ya kujengwa upya nyumba hii ya Mungu.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
But in the first year of Cyrus the king of Babylon the same king Cyrus made a decree to build this house of God.
In Context
12Lakini kwa sababu baba zetu walimkasirisha Mungu wa mbinguni, basi aliwatia mkononi mwa Nebukadneza, Mkaldayo, mfalme wa Babeli, ambaye aliliharibu Hekalu hili na kuwaondoa watu na kuwapeleka uhamishoni huko Babeli.
14Yeye hata aliviondoa vyombo vya dhahabu na fedha vya nyumba ya Mungu, kutoka Hekalu la Babeli ambavyo Nebukadneza alikuwa amevichukua kutoka ndani ya Hekalu huko Yerusalemu na kuvileta katika Hekalu la Babeli. “Vyombo hivyo Mfalme Koreshi alimkabidhi mtu aliyeitwa Sheshbaza, ambaye Koreshi alikuwa amemteua awe mtawala,
Read all of Ezra 5
Cross References
Ezra 1:3Yeyote wa watu wake miongoni mwenu, Mungu wake na awe pamoja naye, wacha apande kwenda Yerusalemu katika Yuda na kujenga Hekalu la Bwana, Mungu wa Israeli, Mungu aliyeko huko Yerusalemu.
Isaiah 44:28nisemaye kuhusu Koreshi, ‘Yeye ni mchungaji wangu, 2 naye atatimiza yote yanipendezayo; 2 atauambia Yerusalemu, “Ukajengwe tena,” 2 na kuhusu Hekalu, “Misingi yake na iwekwe.” ’
This Verse In Other Editions
Study Ezra 5:13