Genesis 29:1
Kisha Yakobo akaendelea na safari yake na akafika kwenye nchi za mataifa ya mashariki.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
Then Jacob went on his journey, and came into the land of the people of the east.
In Context
Cross References
Genesis 24:10Ndipo huyo mtumishi akachukua ngamia kumi miongoni mwa ngamia za bwana wake, akaondoka, akiwa amechukua aina zote za vitu vizuri kutoka kwa bwana wake. Akaelekea Aramu-Naharaimu + 24:10 Yaani Mesopotamia ya Kaskazini-Magharibi. na kushika njia kwenda mji wa Nahori.
Genesis 25:20Isaki alikuwa na umri wa miaka arobaini alipomwoa Rebeka binti Bethueli Mwaramu kutoka Padan-Aramu, nduguye Labani Mwaramu.
Genesis 35:1Kisha Mungu akamwambia Yakobo, “Panda uende Betheli ukakae huko na ukamjengee Mungu madhabahu huko, Yeye aliyekutokea ulipokuwa unamkimbia Esau ndugu yako.”
Numbers 23:7Ndipo Balaamu akasema ujumbe wake: 1 “Balaki amenileta kutoka Aramu, 2 mfalme wa Moabu kutoka milima ya mashariki. 1 Akasema, ‘Njoo, unilaanie Yakobo; 2 njoo unishutumie Israeli.’ 1
Judges 6:33Basi Wamidiani wote, Waamaleki na mataifa mengine ya mashariki wakaunganisha majeshi yao, wakavuka ngʼambo ya Yordani na kupiga kambi katika Bonde la Yezreeli.
Judges 8:10Wakati huu Zeba na Salmuna walikuwa Karkori wakiwa na jeshi lenye watu wapatao 15,000 wale wote waliokuwa wamesalia wa mataifa ya mashariki, kwa kuwa watu wapatao 120,000 wenye panga walikuwa wameuawa.