Genesis 39:4
Yosefu alipata kibali machoni pa Potifa, akamfanya mhudumu wake. Potifa akamweka kuwa msimamizi wa nyumba yake, naye akamkabidhi kuwa mwangalizi wa kila kitu alichokuwa nacho.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Genesis 18:3Akasema, “Kama nimepata kibali machoni penu, ee bwana wangu, usimpite mtumishi wako.
Genesis 24:2Akamwambia mtumishi wake mkuu wa vitu vyote katika nyumba yake, yule aliyekuwa msimamizi wa vitu vyote alivyokuwa navyo, “Weka mkono wako chini ya paja langu,
Genesis 33:8Esau akauliza, “Una maana gani kuhusu makundi hayo yote niliyokutana nayo?” Akasema, “Ni ili kupata kibali machoni pako, bwana wangu.”
Genesis 39:8Lakini Yosefu akakataa. Akamwambia yule mwanamke, “Mimi nikiwa katika uongozi, bwana wangu hahusiki na kitu chochote katika nyumba hii, kila kitu alicho nacho amenikabidhi.
Genesis 41:40Wewe utakuwa msimamizi wa jumba langu la kifalme, na watu wangu wote watatii amri zako. Ni kuhusu kiti cha ufalme tu nitakuwa mkuu kuliko wewe.” 1 Yosefu Msimamizi Wa Misri
1 Samuel 2:26Naye kijana Samweli akaendelea kukua katika kimo, akimpendeza Bwana na wanadamu. 1 Unabii Dhidi Ya Nyumba Ya Eli