Genesis 40:5
kila mmoja wa hao wawili waliokuwa wamewekwa gerezani, yaani mnyweshaji na mwokaji wa mfalme wa Misri, waliota ndoto usiku mmoja, na kila ndoto ilikuwa na maana yake tofauti.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
6Yosefu alipowajia asubuhi yake, akawaona kwamba walikuwa na huzuni.
Cross References
Genesis 20:3Lakini Mungu akamjia Abimeleki katika ndoto wakati wa usiku na kumwambia, “Wewe ni kama mfu kwa sababu ya huyu mwanamke uliyemchukua; yeye ni mke wa mtu.”
Genesis 40:8Wakamjibu, “Sisi sote tuliota ndoto, lakini hapakuwa na mtu yeyote wa kuzifasiri.” Ndipo Yosefu akawaambia, “Je, kufasiri ndoto si kazi ya Mungu? Niambieni ndoto zenu.”
Genesis 41:5Farao akaingia usingizini tena akaota ndoto ya pili: Akaona masuke saba ya nafaka, yenye afya na mazuri, yanakua katika bua moja.
Numbers 12:6Bwana akasema, “Sikilizeni maneno yangu: 1 “Akiwapo nabii wa Bwana miongoni mwenu, 2 nitajifunua kwake kwa maono, 2 nitanena naye katika ndoto. 1
Esther 6:1Usiku ule mfalme hakupata usingizi, hivyo akaagiza aletewe kitabu cha kumbukumbu za matukio ya utawala wake, asomewe.
Daniel 2:1Katika mwaka wa pili wa utawala wake, Nebukadneza aliota ndoto. Mawazo yake yakasumbuka na hakuweza kulala.