Isaiah 10:13
Kwa kuwa anasema: 1 “ ‘Kwa nguvu za mkono wangu nimefanya hili, 2 kwa hekima yangu, kwa sababu nina ufahamu. 1 Niliondoa mipaka ya mataifa, 2 niliteka nyara hazina zao, 1 kama yeye aliye shujaa 2 niliwatiisha wafalme wao. 1
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Judges 7:2Bwana akamwambia Gideoni, “Jeshi lililo pamoja nawe ni kubwa sana kwa mimi kuwatia Wamidiani mikononi mwao. Ili kwamba Israeli asije akajisifu juu yangu akisema, ‘Mkono wangu ndio ulioniokoa,
2 Kings 16:8Naye Ahazi akachukua fedha na dhahabu zilizopatikana ndani ya Hekalu la Bwana na katika hazina ya jumba la mfalme, na kuzituma kama zawadi kwa mfalme wa Ashuru.
2 Kings 17:24Mfalme wa Ashuru akawaleta watu kutoka Babeli, Kutha, Ava, Hamathi na Sefarvaimu na kuwaweka katika miji ya Samaria badala ya Waisraeli. Wakaimiliki Samaria na kuishi katika miji yake.
2 Kings 18:15Basi Hezekia akampa fedha yote iliyopatikana ndani ya Hekalu la Bwana na katika hazina ya jumba la mfalme.
2 Kings 19:22Ni nani uliyemtukana na kumkufuru? 2 Ni nani uliyeinua sauti yako dhidi yake, 1 na kumwinulia macho yako kwa kiburi? 2 Ni dhidi ya yule Aliye Mtakatifu wa Israeli! 1
1 Chronicles 5:26Kwa hiyo Mungu wa Israeli akaiamsha roho ya Pulu, mfalme wa Ashuru (ambaye pia alijulikana kama Tiglath-Pileseri), ambaye aliwachukua Wareubeni, Wagadi na nusu ya kabila la Manase kwenda uhamishoni. Akawapeleka huko Hala, Habori, Hara na mto Gozani, ambako wamekaa mpaka leo.