Isaiah 37:36
Ndipo malaika wa Bwana akaenda, akawaua wanajeshi 185,000 katika kambi ya Waashuru. Wenzao walipoamka asubuhi yake, walikuta maiti kila mahali!
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
35“Nitaulinda mji huu na kuuokoa, 2 kwa ajili yangu mwenyewe, 2 na kwa ajili ya Daudi mtumishi wangu!”
37Basi Senakeribu mfalme wa Ashuru akavunja kambi na kuondoka. Akarudi Ninawi na kukaa huko.
Cross References
Exodus 12:23Bwana apitapo katika nchi yote kuwapiga Wamisri, ataiona damu juu ya vizingiti na kwenye miimo ya milango, naye atapita juu, wala hatamruhusu mwangamizi kuingia katika nyumba zenu na kuwapiga ninyi.
2 Samuel 24:16Malaika aliponyoosha mkono wake ili kuangamiza Yerusalemu, Bwana akahuzunika kwa sababu ya maafa, akamwambia yule malaika aliyekuwa anawadhuru watu, “Yatosha! Rudisha mkono wako.” Wakati huo malaika wa Bwana alikuwa kwenye sakafu ya kupuria ya Arauna, + 24:16 Pia anaitwa Ornani kwa Kiebrania. Myebusi.
1 Chronicles 21:12miaka mitatu ya njaa, au miezi mitatu ya kushindwa na adui zako, ukipatwa na upanga wao, au siku tatu za upanga wa Bwana, yaani, siku tatu za tauni katika nchi na malaika wa Bwana akiangamiza kila mahali katika Israeli.’ Sasa basi, amua jinsi nitakavyomjibu yeye aliyenituma.”
2 Chronicles 32:21Naye Bwana akamtuma malaika ambaye aliangamiza wanajeshi wote, na viongozi na maafisa katika kambi ya mfalme wa Ashuru. Kwa hiyo, mfalme wa Ashuru akarudi nchini mwake kwa aibu. Naye alipokwenda katika hekalu la mungu wake, baadhi ya watoto wake wakamuua kwa upanga.
Job 24:24Kwa kitambo kidogo hutukuka, hatimaye hutoweka; 2 hushushwa na kukusanywa kama wengine wote, 2 hukatwa kama masuke ya nafaka. 1
Psalms 35:5Wawe kama makapi yapeperushwayo na upepo, 2 malaika wa Bwana akiwafukuza. 1