Isaya 42:24
Ni nani aliyemtoa Yakobo kuwa mateka, 2 na Israeli kwa wateka nyara? 1 Je, hakuwa yeye, Bwana, 2 ambaye tumetenda dhambi dhidi yake? 1 Kwa kuwa hawakufuata njia zake, 2 hawakutii sheria zake. 1
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
23Ni nani miongoni mwenu atakayesikiliza hili, 2 au atakayezingatia kwa makini katika wakati ujao? 1
Cross References
Deuteronomy 28:49Bwana ataleta taifa dhidi yako kutoka mbali, kutoka miisho ya dunia, kama tai ashukiavyo mawindo chini, taifa ambalo hutaijua lugha yake,
Judges 2:14Hivyo hasira ya Bwana ikawaka juu ya Israeli, naye akawatia mikononi mwa wavamizi waliowateka nyara. Akawauza katika mikono ya adui zao pande zote, hivyo hawakuweza tena kuwazuia adui zao.
Judges 10:7hivyo hasira ya Bwana ikawaka dhidi ya Israeli, naye akawatia mikononi mwa Wafilisti na Waamoni,
2 Chronicles 36:17Mungu akamwinua dhidi yao mfalme wa Wakaldayo, aliyewaua vijana wao wa kiume kwa upanga ndani ya mahali patakatifu, ambaye hakumbakiza kijana mwanaume wala kijana mwanamke, wazee wala vikongwe. Mungu akawatia wote mikononi mwa Nebukadneza.
Psalms 81:12Basi niliwaacha katika ukaidi wa mioyo yao 2 wafuate mashauri yao wenyewe. 1
Isaiah 10:5“Ole kwa Ashuru, fimbo ya hasira yangu, 2 ambaye mkononi mwake ana rungu ya ghadhabu yangu! 1