Isaiah 49:2
Akafanya kinywa changu kuwa kama upanga ulionolewa, 2 katika uvuli wa mkono wake akanificha; 1 akanifanya kuwa mshale uliosuguliwa, 2 na kunificha katika podo lake. 1
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
3Akaniambia, “Wewe u mtumishi wangu, 2 Israeli, ambaye katika yeye 2 nitaonyesha utukufu wangu.” 1
Cross References
Psalms 45:2Wewe ni bora kuliko watu wengine wote 2 na midomo yako imepakwa neema, 2 kwa kuwa Mungu amekubariki milele. 1
Isaiah 11:4bali kwa uadilifu atahukumu wahitaji, 2 kwa haki ataamua wanyenyekevu wa dunia. 1 Ataipiga dunia kwa fimbo ya kinywa chake, 2 kwa pumzi ya midomo yake atawaua waovu. 1
Isaiah 50:4Bwana Mwenyezi amenipa ulimi uliofundishwa, 2 ili kujua neno limtegemezalo aliyechoka. 1 Huniamsha asubuhi kwa asubuhi, 2 huamsha sikio langu lisikie kama mtu afundishwaye. 1
Isaiah 61:1Roho wa Bwana Mwenyezi yu juu yangu, 2 kwa sababu Bwana amenitia mafuta 2 kuwahubiria maskini habari njema. 1 Amenituma kuwaganga waliovunjika moyo, 2 kuwatangazia mateka uhuru wao, 1 na hao waliofungwa 2 habari za kufunguliwa kwao; 1
Jeremiah 15:19Kwa hiyo hili ndilo asemalo Bwana: 1 “Kama ukitubu, nitakurejeza 2 ili uweze kunitumikia; 1 kama ukinena maneno yenye maana, 2 wala si ya upuzi, 2 utakuwa mnenaji wangu. 1 Watu hawa ndio watakaokugeukia, 2 wala si wewe utakayewageukia wao. 1
Luke 23:46Yesu akapaza sauti yake akasema, “Baba, mikononi mwako naikabidhi roho yangu.” Baada ya kusema haya, akakata roho.