Yeremia 17:4
Kwa kosa lako mwenyewe utaupoteza 2 urithi niliokupa. 1 Nitakufanya mtumwa wa adui zako 2 katika nchi usiyoijua, 1 kwa kuwa umeiwasha hasira yangu, 2 nayo itawaka milele.”
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Leviticus 26:31Nitaifanya miji yenu kuwa magofu, na kuharibu mahali patakatifu penu pa kuabudia, nami sitapendezwa na harufu nzuri ya sadaka zenu.
Deuteronomy 28:25Bwana atakufanya ushindwe mbele ya adui zako. Utawajia kwa njia moja lakini utawakimbia mbele yao kwa njia saba, nawe utakuwa kitu cha kuchukiza kwa falme zote za dunia.
Deuteronomy 29:26Walienda zao na kuabudu miungu mingine na kuisujudia, miungu wasioijua, miungu ambayo Mungu hakuwapa.
Joshua 23:15Lakini kama vile kila ahadi njema ya Bwana Mungu wenu imekuwa kweli, vivyo hivyo Bwana ataleta maovu yote kama alivyo onya, mpaka awe amewaangamiza kutoka nchi hii nzuri aliyowapa.
2 Kings 25:21Huko Ribla, katika nchi ya Hamathi, mfalme wa Babeli akaamuru wanyongwe. Hivyo Yuda wakaenda utumwani, mbali na nchi yao.
Isaiah 5:25Kwa hiyo hasira ya Bwana inawaka dhidi ya watu wake, 2 mkono wake umeinuliwa na anawapiga. 1 Milima inatetemeka, 2 maiti ni kama takataka kwenye barabara. 1 Hata kwa haya yote, hasira yake haijageukia mbali, 2 mkono wake bado umeinuliwa juu. 1