Yeremia 19:4
Kwa kuwa wameniacha na kupafanya mahali hapa kuwa pa miungu ya kigeni. Wameiteketezea sadaka miungu ambayo wao wala baba zao wala wafalme wa Yuda kamwe hawakuijua, nao wamelijaza eneo hili kwa damu isiyo na hatia.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Deuteronomy 13:6Kama ndugu yako hasa, au mwanao au binti yako, au mke umpendaye, au rafiki yako wa karibu sana akikushawishi kwa siri, akisema, “Na twende tukaabudu miungu mingine” (miungu ambayo ninyi wala baba zenu hamkuifahamu,
Deuteronomy 28:20Bwana ataleta laana juu yako, fadhaa na kukaripiwa katika kila kitu unachokigusa kwa mkono wako, mpaka uwe umeharibiwa na kuangamizwa ghafula kwa ajili ya maovu uliyoyafanya kwa kumwacha yeye.
Deuteronomy 28:64Kisha Bwana atawatawanya miongoni mwa mataifa yote, kutoka mwisho mmoja wa dunia hadi mwingine. Huko mtaabudu miungu mingine, miungu ya miti na ya mawe, ambayo ninyi wala baba zenu hamkuijua.
Deuteronomy 32:15Yeshuruni + 32:15 Yeshuruni maana yake ni Yeye aliye mnyofu, yaani Israeli (ona pia Kum 33:26; Isa 44:2 ). alinenepa na kupiga teke; 2 alikuwa na chakula tele, 2 akawa mzito na akapendeza sana. 1 Akamwacha Mungu aliyemuumba, 2 na kumkataa Mwamba Mwokozi wake. 1
Judges 5:8Walipochagua miungu migeni, 2 vita vilikuja katika malango ya mji, 1 hapakuonekana ngao wala mkuki 2 miongoni mwa mashujaa 40,000 katika Israeli. 1
2 Kings 21:16Zaidi ya hayo, Manase pia alimwaga damu nyingi isiyo na hatia, hivi kwamba aliijaza Yerusalemu kutoka mwanzo hadi mwisho, mbali na dhambi ambayo alikuwa amesababisha Yuda kufanya, na hivyo wakatenda maovu machoni pa Bwana.