Yeremia 46:28
Usiogope, ee Yakobo mtumishi wangu, 2 kwa maana mimi niko pamoja nawe,” 2 asema Bwana. 1 “Ingawa nitayaangamiza kabisa mataifa yote 2 ambayo miongoni mwake nimekutawanya, 2 sitakuangamiza wewe kabisa. 1 Nitakurudi, lakini kwa haki tu, 2 wala sitakuacha kabisa bila kukuadhibu.”
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Joshua 1:5Hakuna mtu yeyote atakayeweza kushindana na wewe siku zote za maisha yako. Kama vile nilivyokuwa pamoja na Mose, ndivyo nitakavyokuwa pamoja na wewe, sitakuacha wala sitakupungukia.
Psalms 46:7Bwana Mwenye Nguvu Zote yu pamoja nasi, 2 Mungu wa Yakobo ni ngome yetu. 1
Isaiah 8:9Inueni kilio cha vita, enyi mataifa, 2 na mkavunjwevunjwe! 2 Sikilizeni, enyi nyote nchi za mbali. 1 Jiandaeni kwa vita, nanyi mkavunjwevunjwe! 2 Jiandaeni kwa vita, nanyi mkavunjwevunjwe! 1
Isaiah 27:9Kwa hili, basi, hatia ya Yakobo itafanyiwa upatanisho, 2 nalo hili litakuwa matunda ya utimilizo wa kuondolewa kwa dhambi yake: 1 Wakati atakapoyafanya mawe yote ya madhabahu 2 kuwa kama mawe ya chokaa yaliyopondwa vipande vipande, 1 hakuna nguzo za Ashera au madhabahu za kufukizia uvumba 2 zitakazobaki zimesimama. 1
Isaiah 43:2Unapopita kwenye maji makuu, 2 nitakuwa pamoja nawe, 1 unapopita katika mito ya maji, 2 hayatakugharikisha. 1 Utakapopita katika moto, 2 hutaungua, 2 miali ya moto haitakuunguza. 1
Jeremiah 1:19Watapigana nawe lakini hawatakushinda, kwa kuwa niko pamoja nawe, nami nitakuokoa,” asema Bwana.