Joel 2:14
Ni nani ajuaye? Yeye aweza kugeuka na kuwa na huruma 2 na kuacha baraka nyuma yake: 1 sadaka za nafaka na sadaka za vinywaji 2 kwa ajili ya Bwana Mungu wenu. 1
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
15Pigeni tarumbeta katika Sayuni, 2 tangazeni saumu takatifu, 2 liiteni kusanyiko takatifu. 1
Cross References
Joshua 14:12Basi nipe nchi hii ya vilima, ambayo Bwana aliniahidi siku ile. Wewe mwenyewe ulisikia wakati ule kwamba Waanaki walikuwako huko na miji yao ilikuwa mikubwa na yenye maboma, lakini, kwa msaada wa Bwana, nitawafukuza watoke huko kama vile alivyonena.”
2 Samuel 12:22Akajibu, “Wakati mtoto alipokuwa bado yungali hai, nilifunga na kulia. Nilifikiri, ‘Nani ajuaye? Bwana aweza kunirehemu ili kumwacha mtoto aishi.’
2 Kings 19:4Yamkini Bwana, Mungu wako atayasikia maneno ya jemadari wa jeshi, ambaye bwana wake, mfalme wa Ashuru, amemtuma kumdhihaki Mungu aliye hai, tena kwamba atamkemea kwa maneno ambayo Bwana, Mungu wako ameyasikia. Kwa hiyo omba kwa ajili ya mabaki ambao bado wako.”
Jeremiah 26:3Huenda watasikiliza, na kila mmoja akageuka kutoka njia yake mbaya. Kisha nitawahurumia na kuacha kuwaletea maafa niliyokuwa ninapanga kwa sababu ya maovu waliyofanya.
Joel 1:13Vaeni nguo ya gunia, enyi makuhani, muomboleze; 2 pigeni yowe, enyi mnaohudumu madhabahuni. 1 Njooni, vaeni nguo ya gunia usiku kucha, 2 enyi mnaohudumu mbele za Mungu wangu; 1 kwa kuwa sadaka za nafaka na sadaka za kinywaji 2 zimezuiliwa kufika katika nyumba ya Mungu wenu. 1
Amos 5:15Yachukieni maovu, yapendeni mema; 2 dumisheni haki mahakamani. 1 Yamkini Bwana Mungu Mwenye Nguvu Zote 2 atawahurumia mabaki ya Yosefu.