John 12:42
Lakini wengi miongoni mwa viongozi wa Wayahudi walimwamini, lakini kwa sababu ya Mafarisayo hawakukiri waziwazi kwa maana waliogopa kufukuzwa katika masinagogi.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
41Isaya alisema haya alipoona utukufu wa Yesu na kunena habari zake.
43Wao walipenda sifa za wanadamu kuliko sifa zitokazo kwa Mungu. 1 Amwaminiye Yesu Hatabaki Gizani
Cross References
Isaiah 51:7“Nisikieni, ninyi mnaojua lililo sawa, 2 ninyi watu ambao mna sheria yangu mioyoni mwenu: 1 Msiogope mashutumu ya wanadamu 2 wala msitiwe hofu na matukano yao. 1
Isaiah 66:5Sikieni neno la Bwana, 2 ninyi mtetemekao kwa neno lake: 1 “Ndugu zenu wanaowachukia ninyi 2 na kuwatenga ninyi kwa sababu ya Jina langu, wamesema, 1 ‘ Bwana na atukuzwe, 2 ili tupate kuona furaha yenu!’ 2 Hata sasa wataaibika. 1
Matthew 26:69Wakati huu Petro alikuwa amekaa nje uani. Mtumishi mmoja wa kike akamjia na kumwambia, “Wewe pia ulikuwa pamoja na Yesu wa Galilaya.”
Luke 12:8“Ninawaambia kwamba yeyote atakayenikiri mbele ya watu, Mwana wa Adamu naye atamkiri mbele za malaika wa Mungu.
John 7:13Lakini hakuna mtu yeyote aliyemsema waziwazi kumhusu kwa sababu ya kuwaogopa Wayahudi. 1 Yesu Afundisha Kwenye Sikukuu
John 9:22Wazazi wake walisema hivi kwa sababu waliwaogopa Wayahudi kwani walikuwa wamekubaliana kuwa mtu yeyote atakayemkiri Yesu kuwa ndiye Kristo + 9:22 Kristo maana yake ni Masiya , yaani Aliyetiwa mafuta. atafukuzwa kutoka sinagogi.