John 19:15
Wao wakapiga kelele, “Mwondoe! Mwondoe! Msulubishe!” Pilato akawauliza, “Je, nimsulubishe mfalme wenu?” Wale viongozi wa makuhani wakamjibu, “Sisi hatuna mfalme mwingine ila Kaisari.”
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Genesis 49:10Fimbo ya ufalme haitaondoka kwa Yuda, 2 wala fimbo ya mtawala kati ya miguu yake, 1 hadi aje yeye ambaye milki ni yake, 2 ambaye utii wa mataifa ni wake. 1
Luke 23:18Ndipo watu wote wakapiga kelele kwa pamoja, “Mwondoe mtu huyo! Tufungulie Baraba!”
John 19:6Wale viongozi wa makuhani na maafisa walipomwona, wakapiga kelele wakisema, “Msulubishe! Msulubishe!” Pilato akawaambia, “Mchukueni ninyi mkamsulubishe, mimi sioni hatia juu yake.”
Acts 22:22Ule umati wa watu wakamsikiliza Paulo mpaka aliposema neno hilo, ndipo wakapaza sauti zao na kupiga kelele wakisema, “Mwondoeni duniani, hafai kuishi!”