John 20:16
Yesu akamwita, “Maria!” Ndipo Maria akamgeukia Yesu na kusema naye kwa Kiebrania, “Rabboni!” (maana yake Mwalimu).
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Genesis 22:1Baadaye Mungu akamjaribu Abrahamu. Akamwambia, “Abrahamu!” Abrahamu akajibu, “Mimi hapa.”
Genesis 45:12“Mnaweza kujionea wenyewe, hata ndugu yangu Benyamini, kwamba hakika ni mimi ninayezungumza nanyi.
Exodus 33:17Bwana akamwambia Mose, “Nitakufanyia jambo lile uliloomba, kwa sababu ninapendezwa nawe, nami ninakujua kwa jina lako.”
1 Samuel 3:10Bwana akaja akasimama hapo, akiita kama mara zile nyingine, “Samweli! Samweli!” Kisha Samweli akasema, “Nena Bwana, kwa kuwa mtumishi wako anasikiliza.”
Song of Solomon 3:4Kitambo kidogo tu baada ya kuwapita 2 nilimpata yule moyo wangu umpendaye. 1 Nilimshika na sikumwachia aende 2 mpaka nilipomleta katika nyumba ya mama yangu, 2 katika chumba cha yule aliyenichukua mimba. 1
Isaiah 43:1Lakini sasa hili ndilo asemalo Bwana, 2 yeye aliyekuumba, ee Yakobo, 2 yeye aliyekuhuluku, ee Israeli: 1 “Usiogope kwa maana nimekukomboa, 2 nimekuita wewe kwa jina lako, wewe u wangu. 1