John 7:38
Yeyote aniaminiye mimi, kama Maandiko yasemavyo, vijito vya maji ya uzima vitatiririka ndani mwake.”
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Deuteronomy 18:15Bwana Mungu wenu atawainulia nabii kama mimi kutoka miongoni mwa ndugu zenu wenyewe. Msikilizeni yeye.
Proverbs 10:11Kinywa cha mwenye haki ni chemchemi ya uzima, 2 lakini jeuri hufunika kinywa cha mwovu. 1
Isaiah 12:3Kwa furaha mtachota maji 2 kutoka visima vya wokovu.
Isaiah 58:11Bwana atakuongoza siku zote, 2 atayatosheleza mahitaji yako katika nchi kame, 2 naye ataitia nguvu mifupa yako. 1 Utakuwa kama bustani iliyonyweshwa vizuri, 2 kama chemchemi ambayo maji yake hayakauki kamwe. 1
Ezekiel 47:1Yule mtu akanirudisha mpaka kwenye ingilio la Hekalu, nami nikaona maji yakitoka chini ya kizingiti cha Hekalu yakitiririkia upande wa mashariki (kwa maana upande wa mbele wa Hekalu ulielekea mashariki). Maji yalikuwa yakitoka chini upande wa kusini wa Hekalu, kusini mwa madhabahu.
John 4:10Yesu akajibu akamwambia, “Kama ungelijua karama ya Mungu, naye ni nani anayekuambia, Nipe maji ninywe, wewe ungelimwomba yeye, naye angelikupa maji yaliyo hai.”