John 7:37
Siku ile ya mwisho ya Sikukuu, siku ile kuu, wakati Yesu akiwa amesimama huko, akapaza sauti yake akasema, “Kama mtu yeyote anaona kiu na aje kwangu anywe.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
38Yeyote aniaminiye mimi, kama Maandiko yasemavyo, vijito vya maji ya uzima vitatiririka ndani mwake.”
Cross References
Leviticus 23:36Kwa siku saba toeni sadaka kwa Bwana za kuteketezwa kwa moto. Kwenye siku ya nane fanyeni kusanyiko takatifu, na mtoe sadaka kwa Bwana ya kuteketezwa kwa moto. Ni kusanyiko la mwisho, msifanye kazi zenu za kawaida.
Numbers 29:35“ ‘Katika siku ya nane mtakuwa na kusanyiko, na msifanye kazi ya kawaida.
Nehemiah 8:18Siku baada ya siku, kuanzia siku ya kwanza hadi ya mwisho, Ezra alisoma kutoka kwenye kile Kitabu cha Sheria ya Mungu. Wakaiadhimisha sikukuu ile kwa siku saba, nayo siku ya nane, kufuatana na maagizo, kulikuwa na kusanyiko maalum.
Psalms 42:2Nafsi yangu inamwonea Mungu kiu, Mungu aliye hai. 2 Ni lini nitaweza kwenda kukutana na Mungu? 1
Psalms 143:6Nanyoosha mikono yangu kwako, 2 nafsi yangu inakuonea kiu kama ardhi kame. 1
Proverbs 8:1Je, hekima haitani? 2 Je, ufahamu hapazi sauti? 1