John 9:24
Hivyo kwa mara ya pili wakamwita yule aliyekuwa kipofu, nao wakamwambia, “Mpe Mungu utukufu! Sisi tunafahamu kuwa mtu huyu aliyekuponya ni mwenye dhambi.”
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
23Kwa hiyo wazazi wake wakasema, “Yeye ni mtu mzima. Muulizeni.”
Cross References
1 Samuel 6:5Tengenezeni mifano ya majipu na ya panya wale wanaoharibu nchi yenu, nanyi mheshimuni Mungu wa Israeli. Labda ataondoa mkono wake kutoka kwenu na kwa miungu yenu na nchi yenu.
Isaiah 66:5Sikieni neno la Bwana, 2 ninyi mtetemekao kwa neno lake: 1 “Ndugu zenu wanaowachukia ninyi 2 na kuwatenga ninyi kwa sababu ya Jina langu, wamesema, 1 ‘ Bwana na atukuzwe, 2 ili tupate kuona furaha yenu!’ 2 Hata sasa wataaibika. 1
Luke 7:39Yule Farisayo aliyemwalika Yesu alipoona yanayotendeka, akawaza moyoni mwake, “Kama huyu mtu angekuwa nabii, angejua kwamba ni nani anayemgusa, na kwamba yeye ni mwanamke wa namna gani, na ya kuwa huyu mwanamke ni mwenye dhambi.”
Luke 19:7Watu wote walipoona hivyo, wakaanza kunungʼunika wakisema, “Amekwenda kuwa mgeni wa ‘mtu mwenye dhambi.’ ”
John 8:46Je, kuna yeyote miongoni mwenu awezaye kunithibitisha kuwa mwenye dhambi? Kama nawaambia yaliyo kweli, mbona hamniamini?
John 9:16Baadhi ya Mafarisayo wakasema, “Huyu mtu hatoki kwa Mungu, kwa sababu hashiki Sabato.” Lakini wengine wakasema, “Awezaje mtu mwenye dhambi kufanya miujiza kama hii?” Wakagawanyika.