Yoshua 1:4
Nchi yenu itaenea kuanzia jangwa hili hadi Lebanoni, tena kuanzia mto mkubwa wa Frati, yaani nchi yote ya Wahiti, hadi Bahari ile Kubwa + 1:4 Yaani Bahari ya Mediterania. iliyoko upande wa magharibi.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
3Kila mahali nyayo za miguu yenu zitakapokanyaga nimewapa, kama vile nilivyomwahidi Mose.
Cross References
Exodus 23:31“Nitaweka mipaka ya nchi yako kuanzia Bahari ya Shamu hadi Bahari ya Wafilisti, na kuanzia jangwani hadi Mto Frati. Nitawatia watu wanaoishi katika nchi hizo mikononi mwako, nawe utawafukuza watoke mbele yako.
Deuteronomy 1:7Vunjeni kambi, msonge mbele kuelekea nchi ya vilima ya Waamori; nendeni kwa watu wote ambao ni majirani wa Araba, katika milima, upande wa magharibi chini ya vilima, katika Negebu na kandokando ya pwani, mpaka nchi ya Wakanaani hadi Lebanoni, na kufika mto mkubwa Frati.
Deuteronomy 11:24Kila mahali mtakapoweka mguu wenu patakuwa penu: Nchi yenu itaenea kutoka jangwa la Lebanoni, na kutoka mto wa Frati hadi bahari ya magharibi + 11:24 Yaani Bahari ya Mediterania.
1 Chronicles 5:9Kwa upande wa mashariki walienea hadi pembeni mwa jangwa linaloenea mpaka kwenye Mto Frati, kwa sababu mifugo yao ilikuwa imeongezeka huko Gileadi. 2