Joshua 21:45
Hakuna hata mojawapo ya ahadi nzuri ya Bwana kwa nyumba ya Israeli ambayo haikutimia; kila moja ilitimia.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Numbers 23:19Mungu si mtu, hata aseme uongo, 2 wala yeye si mwanadamu, hata ajute. 1 Je, anasema, kisha asitende? 2 Je, anaahidi, asitimize? 1
1 Samuel 3:19Bwana alikuwa pamoja na Samweli alipokuwa akikua, na hakuacha hata moja ya maneno yake lianguke chini.
1 Kings 8:20“ Bwana ametimiza ahadi aliyoiweka: Nimeingia mahali pa Daudi baba yangu na sasa ninakikalia kiti cha ufalme cha Israeli, kama vile Bwana alivyoahidi, nami nimejenga Hekalu kwa ajili ya Jina la Bwana, Mungu wa Israeli.
1 Kings 8:56“Ahimidiwe Bwana, aliyewapa pumziko watu wake Israeli kama vile alivyokuwa ameahidi. Hakuna hata neno moja lililopunguka kati ya ahadi zote nzuri alizozitoa kupitia mtumishi wake Mose.
Isaiah 48:3Nilitoa unabii mambo ya kwanza tangu zamani, 2 kinywa changu kiliyatangaza na kuyafanya yajulikane; 2 kisha ghafula nikayatenda, nayo yakatokea. 1
1 Thessalonians 5:24Yeye aliyewaita ni mwaminifu naye atafanya hayo.