Isaiah 48:3
Nilitoa unabii mambo ya kwanza tangu zamani, 2 kinywa changu kiliyatangaza na kuyafanya yajulikane; 2 kisha ghafula nikayatenda, nayo yakatokea. 1
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Joshua 21:45Hakuna hata mojawapo ya ahadi nzuri ya Bwana kwa nyumba ya Israeli ambayo haikutimia; kila moja ilitimia.
Isaiah 10:12Bwana atakapokuwa amemaliza kazi yake yote dhidi ya Mlima Sayuni na Yerusalemu, atasema, “Nitamwadhibu mfalme wa Ashuru kwa ajili ya majivuno ya ukaidi wa moyo wake na kutazama kwa macho yenye dharau.”
Isaiah 37:7Sikiliza! Nitatia roho fulani ndani yake ili kwamba atakaposikia taarifa fulani, atarudi nchi yake mwenyewe, nami huko nitafanya auawe kwa upanga.’ ”
Isaiah 37:36Ndipo malaika wa Bwana akaenda, akawaua wanajeshi 185,000 katika kambi ya Waashuru. Wenzao walipoamka asubuhi yake, walikuta maiti kila mahali!
Isaiah 42:9Tazama, mambo ya kwanza yametokea, 2 nami natangaza mambo mapya; 1 kabla hayajatokea 2 nawatangazia habari zake.” 1 Wimbo Wa Kumsifu Bwana 1
Isaiah 44:7Ni nani basi aliye kama mimi? Yeye na atangaze. 2 Yeye atangaze na kuweka mbele yangu 1 ni kitu gani kilichotokea tangu nilipoumba watu wangu wa kale, 2 tena ni nini kitakachotokea: 2 naam, yeye na atoe unabii ni nini kitakachokuja. 1