Jude 1:7
Vivyo hivyo, Sodoma na Gomora na pia ile miji iliyokuwa kandokando, ambayo kwa jinsi moja na hao, walijifurahisha kwa uasherati na kufuata tamaa za mwili zisizo za asili, waliwekwa wawe mfano kwa kuadhibiwa katika moto wa milele.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Genesis 13:13Basi watu wa Sodoma walikuwa waovu, wakifanya sana dhambi dhidi ya Bwana.
Genesis 19:5Wakamwita Loti wakisema, “Wako wapi wale watu ambao walikuja kwako jioni hii? Watoe nje kwetu ili tuweze kuwalawiti.”
Deuteronomy 29:23Nchi yote itakuwa jaa linaloungua la chumvi na kiberiti: hakutakuwa kilichopandwa, hakutakuwa kinachochipua, wala hakutakuwa mimea inayoota juu yake. Itakuwa kama maangamizo ya Sodoma na Gomora, Adma na Seboimu, ambazo Bwana aliangamiza kwa hasira kali.
Isaiah 13:19Babeli, johari ya falme, 2 utukufu wa kiburi cha Wababeli, + 13:19 Wababeli hapa maana yake ni Wakaldayo. 1 itaangushwa na Mungu 2 kama Sodoma na Gomora. 1
Jeremiah 20:16Mtu huyo na awe kama miji ile 2 ambayo Bwana Mungu 2 aliiangamiza bila huruma. 1 Yeye na asikie maombolezo asubuhi 2 na kilio cha vita adhuhuri. 1
Lamentations 4:6Adhabu ya watu wangu 2 ni kubwa kuliko ile ya Sodoma, 1 ambayo ilipinduliwa ghafula 2 bila kuwepo mkono wa msaada. 1